Serikali kugharamia matibabu ya waliojeruhiwa Oktoba 29

HomeKitaifa

Serikali kugharamia matibabu ya waliojeruhiwa Oktoba 29

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaweka utaratibu wa kugharamikia matibabu ya majeruhi wa ghasia zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ambao bado wanahitaji huduma za matibabu.

Vilevile, amesema Serikali itagharamikia vifaa saidizi pamoja na viungo bandia kwa wale waliopata ulemavu wa kudumu, ili kuwawezesha kumudu mazingira yao ya kila siku.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Rais Samia amesema anatambua kuwa wapo wafanyabiashara wadogo ambao kutokana na uwezo wao hawawezi kumudu gharama za bima kubwa, hivyo kundi hilo litaangaliwa hasara walizopata na kupatiwa faraja stahiki.

Aidha, Rais Samia amevielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili nchi iendelee kuwa salama.

error: Content is protected !!