Kampuni ya DP World imeripoti ongezeko kubwa la mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, likionesha mabadiliko ya msingi katika biashara ya kikanda.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, mizigo ya jumla (general cargo) imeongezeka kutoka tani milioni 1.22 mwaka 2023 hadi tani milioni 2.23 mwaka 2025, sawa na ukuaji wa asilimia 81.
Aidha, mizigo ya magari (RoRo) imeongezeka kwa asilimia 15, huku mizigo ya bulk ikikua kwa asilimia 10.
Elitunu Malamia, Mkuu wa Uhusiano wa kampuni hiyo amesema ongezeko hilo linaonyesha kuimarika kwa mnyororo wa usambazaji na kuongezeka kwa imani ya wafanyabiashara.
Aliongeza kuwa rekodi mpya zimewekwa, ikiwemo kushughulikia makontena 43,803 kwa mwezi Machi 2026, kiwango cha juu kuwahi kufikiwa.
Ukuaji huu unaashiria kuongezeka kwa nafasi ya Tanzania katika biashara ya kimataifa.


