Mapato Bandari ya Dar yaongezeka hadi trilioni 1

HomeKitaifa

Mapato Bandari ya Dar yaongezeka hadi trilioni 1

Kampuni ya DP World imesema maboresho ya ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam yameongeza mapato ya serikali kwa kasi kubwa, huku makusanyo ya kila mwezi kupitia TRA yakipanda kutoka wastani wa Sh milioni 800 hadi zaidi ya Sh trilioni 1.

Mkuu wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Elitunu Malamia, amewambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa ongezeko hilo linatokana na kuimarika kwa ufanisi wa kushughulikia mizigo na kupunguza ucheleweshaji bandarini.

Kwa mujibu wa takwimu, makontena yaliyohudumiwa yameongezeka kutoka 165,545 mwaka 2023 hadi 323,837 mwaka 2025, sawa na ukuaji wa asilimia 96.

Alisema maboresho ya mifumo ya kidijitali, pamoja na uwekezaji wa mitambo na usimamizi bora, yamechangia kuongeza kasi ya huduma na kuvutia biashara zaidi.

Ongezeko hilo linaonesha wazi kuwa ufanisi wa bandari una mchango wa moja kwa moja katika mapato ya taifa na ukuaji wa uchumi.

error: Content is protected !!