Jaji Chande: Hakuna ushahidi wa uwepo wa makaburi ya halaiki

HomeKitaifa

Jaji Chande: Hakuna ushahidi wa uwepo wa makaburi ya halaiki

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uhalifu yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema kupitia taarifa ya wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi, Tume hiyo haijathibitisha madai ya kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la Kondo, Kunduchi, manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Jaji Othman ameyasema hayo leo Aprili 23, 2026, wakati akiwasilisha ripoti ya Tume hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuwepo kwa madai ya makaburi ya halaiki ya watu waliofariki dunia kutokana na vurugu za Oktoba 29, 2025 katika eneo hilo.

Aidha, amesema Tume hiyo imebaini madhara ya kiuchumi yaliyotokana na vurugu hizo, ambapo jumla ya madhara hayo yanafikia shilingi bilioni 125, ikiwemo hasara ya shilingi bilioni 89 kwenye sekta binafsi, na bilioni 36 kwenye mali za umma.

error: Content is protected !!