‘Wagonga wanafunzi’ wafungiwa kamera

HomeKitaifa

‘Wagonga wanafunzi’ wafungiwa kamera

Baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi kugongwa na magari na kupoteza maisha katika Barabara kuu ya Dodoma – Dar es Salaam, Halmashauri ya Chamwino inapanga kufunga kamera katika eneo la Bugiri kwa ajili ya kunasa magari yanayopita kwa mwendo kasi.

Kenneth Yindi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino alibainisha hayo wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa fehda za UVIKO-19, katika shule ya Sekondari ya Bugiri huku akieleza kwamba kata hiyo ina shule sita na barabara kuu imepita katika vijiji vitatu.

“Wanafunzi wengi wanagongwa, magari yanakimbia sana hasa yale ya serikali, wanafunzi na hata wananchi wanapoteza maisha kutokana na ajali za barabarani,” “Tumeshafanya kikao na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani na kupeleka ombi rasmi kwa kutumia wataalamu wa ICT tunafunga kamera nne,” alisema Yindi.

Mkuu wa Mkoa wa Dododma, Anthony Mtaka, alisema suala la kufunga kamera ni jambo zuri kwa kuwa litasaidia kuokoa maisha ya wanafunzi katika shule hizo pamoja na watu wote wanotumia barabara hiyo.

error: Content is protected !!