Rais Samia miongoni mwa mwanawake 100 wenye ushawishi Afrika

HomeKimataifa

Rais Samia miongoni mwa mwanawake 100 wenye ushawishi Afrika

Kampuni ya Avance Media katika toleo lake la tano imetoa orodha ya wanawake 100 wenye ushawishi zaidi barani Afrika kwa mwaka 2023.

Miongoni mwao ni Rais wa Tanzania – Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mtendaji wa Merck Foundation, Seneta – Dk. Rasha Kelej; Waziri Mkuu wa Namibia – Mhe. Saara Kuugongelwa-Amadhila pia Rais wa Mabunge Duniani na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Mwanzilishi wa Avance Media, Prince Akpah, alisisitiza kwamba orodha hiyo inalenga kuangazia wanawake wanaoongoza miradi yenye athari kubwa kote Afrika, wakitumikia kama mfano wa kuigwa kwa kizazi kijacho.

Kampuni imezindua chapisho lake la kila mwaka kwa lengo la kutilia mkazo na kusherehekea jitihada za kuvutia za wanawake wa Kiafrika, ambao wanainspire viongozi wa baadaye wa Afrika.

Vigezo vya uteuzi vilijumuisha: Uongozi na Utendaji Bora, Mafanikio Binafsi, Ahadi ya kushirikiana maarifa, Kuvunja Hali ya Kawaida na kuwa Mwanamke Mwafrika Mwenye Mafanikio.

error: Content is protected !!