Rais Samia : Tanzania inafunguka, Tanzania ni jina kubwa

HomeKitaifa

Rais Samia : Tanzania inafunguka, Tanzania ni jina kubwa

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wazalishaji nchini kuongeza juhudi na kutumia fursa zilizopo nchini ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao lakini pia kuliongezea Taifa kipato.

Amesema hayo alipokuwa akishiriki Hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora (President”s Manufacturer of the year Awards) leo tarehe 17 Desemba, 2023 katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki.

“Nawaomba sana tukaze buti tuendelee na uzalishaji Tanzania inafunguka, Tanzania ni jina kubwa limekuwa ulimwenguni kiasi ambacho kila mtu anataka kuja Tanzania. Na si kukua kwa jina lakini ni kwa sifa zetu.

Serikali inafungua fursa zaidi, serikali inaifungua nchi zaidi na zaidi na katika hivyo wengi wa nje wanakuja ndani lakini furaha yetu ni wa ndani muweze kuwapokea wa nje.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais ameweka wazi kwamba kutokana na maboresho ya sheria za ufanyaji biashara nchini, Tanzania imekuwa kimbilio la wawekezaji wengi kutoka nje kutokana na sera zake rafiki.

“Baada ya marekebisho ya sheria ya kufanya biashara tuko kwenye namba nzuri, tuko kwenye sifa nzuri kila mtu anataka kuwekeza Tanzania. Sasa hivi kuna kinyanganyiro cha Afrika hasa kuhusu malighafi.” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!