Rais Samia aagiza suluhu changamoto ya udanganyifu wa mitihani

HomeKitaifa

Rais Samia aagiza suluhu changamoto ya udanganyifu wa mitihani

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kushughlikiwa kwa changamoto ya udanganyifu wa mitihani inayosababisha Tanzania kuwa na wimbi kubwa la wahitimu wasio na uwezo.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) leo Disemba 12, 2023 jijini Dar es Salaam amesema anatumaini Necta itaishughulikia changamoto hiyo mapema ili kuboresha elimu inayotolewa nchini.

“Changamoto ya wizi wa mitihani lazima itafutiwe mwarobaini katika ngazi yoyote itakayofanyaika…natumaini baada ya leo Wizara itakuja na mikakati mizuri ya kushugulikia suala hili na mtaendelea kuwa wakali zaidi,” amesema Rias Samia.

Awali, Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda, aliwaambia wahudhuriaji kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Necta imedhibiti tatizo hilo kwa kiasi kikubwa na jitihada zaidi zinaendelea kuhakikisha linaisha kabisa.

“Wowote watakaojaribu kuiba mtihani hasa kwa mfumo wa kitaasisi hapana shaka tutawakama tu…tunaendelea kuwa macho kuhakikisha kwamba huko hatuwezi kufika,” amesema Prof. Mkenda.

 

error: Content is protected !!