Tanzania kuwa kitovu cha huduma za maabara za madini Afrika Mashariki na Kati

HomeKitaifa

Tanzania kuwa kitovu cha huduma za maabara za madini Afrika Mashariki na Kati

Ujenzi wa maabara ya kisasa ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) unaendelea kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za upimaji wa madini katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Akikagua maendeleo ya mradi huo uliopo Kizota, Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema maabara hiyo itakuwa na viwango vya kimataifa na kusaidia kutatua changamoto za muda mrefu za wachimbaji, hususan upimaji wa sampuli za madini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa GST, Mhandisi Ally Samaje amesema mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 14.3 unatarajiwa kukamilika Septemba 2027 na utakapokamilika utaweza kuhudumia wateja wa ndani na nje ya nchi kwa huduma bora za maabara za madini.

error: Content is protected !!