Akamatwa kwa kufanya fujo hospitalini baada ya kuzuiwa kuiona familia yake

HomeKitaifa

Akamatwa kwa kufanya fujo hospitalini baada ya kuzuiwa kuiona familia yake

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia Dickson Juma (32) mkazi wa Kiabakari wilayani Butiama kwa tuhuma za kufanya fujo kituo cha afya cha Nyasho kilichopo Manispaa ya Musoma mjini.

Polisi wamesema tukio hilo limetokea leo saa 4 asubuhi ambapo mtuhumiwa alitaka kuwaona mke na watoto wake waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo licha ya muda wa kuona wagonjwa kupita.

Baada ya kuzuiliwa, imeelezwa kuwa mtuhumiwa alianza kufanya fujo na kuvua nguo zote kisha kupanda juu ya mlingoti wa bendera ya taifa, kama njia ya kushinikiza kuruhusiwa kuingia ndani kuona familia yake.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

error: Content is protected !!