Polisi: Kijana aliyekuwa akilumbana na askari alikuwa amelewa

HomeKitaifa

Polisi: Kijana aliyekuwa akilumbana na askari alikuwa amelewa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limetoa ufafanuzi kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana aliyejitambulisha kwa jina la Pilato akilumbana na askari polisi wakati wa ibada.

Kwa mujibu wa polisi, tukio hilo lilitokea Septemba 13, 2026 katika Mlima Itwelele, Manispaa ya Sumbawanga, wakati wa ibada maalum ya Hija iliyohudhuriwa na waumini wa Kanisa Katoliki.

Polisi wamesema kuwa sehemu ya ibada hiyo ilihusisha waumini kuubusu Msalaba na kutoa sadaka. Hata hivyo, wakati ibada ikiendelea, kijana huyo alidaiwa kufika eneo hilo akiwa amelewa na kujaribu kuusogelea Msalaba.

Viongozi wa ibada walimtaka aondoke na kutofuata eneo la Msalaba, lakini alikaidi maelekezo hayo na kuanza kufanya vurugu, hali iliyosababisha askari polisi waliokuwepo kuingilia kati.

Jeshi la Polisi limesema askari huyo alifanikiwa kumuondoa kijana huyo katika eneo la ibada, na shughuli za ibada zikaendelea kwa amani na utulivu.

 

error: Content is protected !!