Rais Mwinyi aunda Kamati ya watu 10 kusimamia mazungumzo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa

HomeKitaifa

Rais Mwinyi aunda Kamati ya watu 10 kusimamia mazungumzo ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameteua kamati ya pamoja ya watu 10 kusimamia mazungumzo ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kati ya CCM na ACT Wazalendo.

Kamati hiyo inajumuisha wajumbe watano kutoka kila chama na imeundwa kufuatia makubaliano yaliyosainiwa kati ya CCM na ACT Wazalendo Julai 9, 2026.

Kamati hiyo itaongozwa kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Ali Shehe, na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi.

Kwa upande wa CCM, wajumbe ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Khalid Salum Mohamed, Mbunge Najma Murtaza Giga, aliyekuwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma na Mohamed Nur Mohamed.

ACT Wazalendo imewakilishwa na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Masoud Ali Mohamed, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Omar Said Shaaban, mgombea mwenza wa uchaguzi wa 2025 Fatma Abdulhabib Fereji na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Said Ali Mbarouk.

Rais Mwinyi pia ameteua makatibu wa pamoja na wajumbe wa sekretarieti ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwalim Ali Mwalim na Seif Khamis Mohamed.

error: Content is protected !!