UDOM Yafunguka tuhuma za rushwa ya ngono zinazomkabili mtumishi wake

HomeKitaifa

UDOM Yafunguka tuhuma za rushwa ya ngono zinazomkabili mtumishi wake

Kufuatia kuzagaa katika mitandao taarifa ya “Mwalimu” wa UDOM kutoka kimapenzi na mwanafunzi wake, soma hapa taarifa iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuhusu tuhuma za ngono zinazomkabili mtumishi wake Bazil Mswahili

“Chuo Kikuu cha Dodoma kinapenda kuutaarifu umma kuwa mnamo tarehe 25 Oktoba, 2021 kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya Mtumishi wake ndugu Petro Bazil Mswahili ambaye ni Mwanataaluma juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma. Baada ya kupokea taarifa hizo. Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na Sheria na kanuni za Utumishi wa Umma.

Vilevile, Mtumishi huyu amemamishwa kufanya majukumu yake yote yakiwemo kufundisha kuanzia tarehe 25 Oktoba, 2021 hadi uchunguzi utakapokamilika Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikichukua hatua stahiki za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma bila kumuonea mtumishi yoyote.

Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote. Pia, Chuo kilaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu. Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.”

error: Content is protected !!