Perfume 5 za kiume zinazochanganya zaidi warembo

HomeElimu

Perfume 5 za kiume zinazochanganya zaidi warembo

Katika mambo ambayo yanasemwa Wanawake huvutiwa nayo sana kutoka kwa Wanaume basi kunukia vizuri kwa mwanaume ni mojawapo. Perfumes zina kitu kama sumaku ya kuvuta warembo. Perfume inaweza pia kuakisi haiba yako, we ni mtu wa aina gani.

Kama kijana, ni muhimu kutambua aina mbalimbali za perfumes ambazo zinaweza kukonga nyonyo za walimbwende na kukuongezea kujiamini.

  1. 1 Million
    Harufu yake ni kama iliki iliyopozwa, haina ukali na haikarahishi pua zako, kwa mbali inaweza kuhisi kama harufu ya ‘citrus’ ama ‘mint’ au harufu ya mvuje uliopoa. Uturi huu usiponusa vizuri, kwa mbali utahisi aina ya maua fulani murua sana kutoka India, maarufu kama Kivumbasi, lakini aina hii ya Kivumbasi ni iliyopoa na si komavu.
  2. Nautica Voyage
    Kwa Dar es Salaam na maeneo yenye joto, basi uturi huu ni mujarabu sana. Utembeapo huathiri eneo unalopita kwa kuacha gumzo kwa harufu yake kama tufaa kwa mchanganyiko wa ambari (amber), miski na virutubisho vingine kutoka kwenye utambazo wa bahari. Nautica inasifika sana kwa harufu yake iliyopoa na kudumu mwilini.
  3. Armaf Club De Nuit Intense
    Unaambiwa hii ni kwa wa vijana wenye kujiamini zaidi, aghalabu sana kwa warembo kutunusha macho yao wasikuangalie kutaka kufahamu ni nani anayenukia harufu nzuri kiasi hicho. Kwa umaridadi kabisa, Perfume hii ina vionjo vya harufu ya nanasi, limao na matunda mengine jamii ya Machungwa. Sio hapo tu, katika mikono tulivu na ustadi wa hali ya juu, uturi huu umechanganywa na maua ya yasmini, waridi pamoja na vanila. NI ngumu kwa mwanamke kukupuuza. Nikuhakikishie, hata muwe Wanaume wangapi mliopaka uturi tofauti, bado Amraf Club De Nuit Intense itachukua nafasi yake.
  4. Creed Aventus
    Balaa jingine hili hapa, hapa kuna mchanganyiko wa harufu nzuri ya zabibi nyeusi, aina ya malimao, matufaa kutoka Ufaransa na harufu nzuri ya mananasi na mchanganyiko wa kivumbasi. Creed Aventus haikwepeki, kwenye kadamnasi ya watu lazima watakuwepo wa kuuliza tu “Perfume gani hiyo”. halafu wewe utakaa kimya kama hujasikia kitu, majibu watayapata ukiondoka au kusimama. Perfume hii bei yake iko juu, ila sisi kazi yetu ni kukujuza tu juu yake, itafute kwani tunaamini utarudi kutushukuru.
  5. Acqua Di Gio
    Perfume hii ndani yake ina mchanganyiko wa maua ya jasmini, rosemarry pamoja harufu jamii ya machungwa kama limao au ndimu. Mgunduzi wa perfume hii ni Mwanamitindo Georgio Armani ambapo wazo lake la utengenezaji wa perfume hii limetokana na kuvutiwa kwake na hali ya mazingira ya Mediterenian katika kisiwa cha Pantelleria. Perfume hii haijawahi kufanya makosa kwenye kukonga nyonyo za walimbwende. Imekuwa na sifa hiyo kutoka kwa kila anayeitumia.
error: Content is protected !!