Ndugu wamnyonga shangazi yao

HomeKitaifa

Ndugu wamnyonga shangazi yao

Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia ndugu wawili kwa tuhuma za kumuua shangazi yao Ndimanya Kahindi kwa kumyonga, Ndimanya alikua mkazi wa kijiji cha Chole Wilayani Misungwi mkoani Mwanza huku tukio hilo likidaiwa kutendeka Novemba 21 mwaka huu majira ya saa 1:30 jioni.

“Kweli tuna washikilia watu wawili ndugu wa familia moja wakituhumiwa kumuua shangazi yao kwa kumnyonga, upelelezi unaendelea kubaini chanzo ni nini cha mauaji hayo”
Kamanda wa Polisi mkoani humo Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa bado chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika lakini uchunguzi unaendelea na ikitokea kuna watu wengine wamehusika watakamatwa na kuunganishwa kwenye kesi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kijijini hapo zilidai marehemu aliuwawa kwa kukabwa shingo na mmoja wa watuhumiwa kisha kumfunga shingoni kwa kutumia kamba ya viatu, Kabla ya tukio hilo kutendeka walikua wakinywa pombe ya kienyeji.

error: Content is protected !!