Je, kuna maisha baada ya kifo?

HomeElimu

Je, kuna maisha baada ya kifo?

 

Einstein anaamini kwamba, hapo ulipo sasa hivi, ulishawahi kufa miaka zaidi ya trilioni nyuma, ni sawa na bado haujazaliwa. Kifo ni kitu ambacho  wengi hatukipendi, na kama tutaishi milele basi dunia itakuwa na shida sana. Tatizo la kufa ni kwamba hakuna ajuaye baada ya kufa ni kitu gani kinatokea huko mbeleni?

Unapoondokewa na mtu wa karibu ni wazi inaumiza sana. Huna cha kufanya, hujui ndugu/mwanao/dada/kaka/mjomba yuko wapi. Kwa kweli ni jambo ambalo kwa 100% liko nje ya uwezo wako.

Sasa hapa ndio dini inapoingia, dini kazi yake kubwa ni kukupa moyo na faraja, dini itakwambia kwamba usiwe na hofu Mungu amependa zaidi, yuko mahala pema peponi na kuna siku utakutana nae. Hakuna cha ziada, kwa maneno haya kwa kuwa umeumbwa na moyo, basi unatulia na kupata nafuu.

Dini itakwambia kuwa kuna moto, pepo, matunda, mito ya maziwa na anasa kibao kwa mbinguni. Kwa moyo binadamu ulivyokuwa na hulka ya kupenda vitu vizuri, basi ni rahisi kuikifu dunia na kuishi maisha ya dini.

Hakuna namna ya kumfariji mzazi aliyefiwa na mwanae, hakuna, zaidi ya kumwambia Mungu amempenda zaidi na atakutana nae. Ambacho wataalamu wanasema ni kibaya kuhusu dini ni kwamba dini inafundisha zaidi kuomboleza na kutunza maumivu.

Dini itakwambia mama yako yuko mbinguni, utaamini lakini inakupa amani lakini hakuna uthibitisho juu ya hili. Hakuna anayefundisha kuwa kifo kipo na kinatokea kweli, na hakuna ajuaye kama kuna maisha baada ya kifo.

Ukiandaa akili yako kuwa utakufa na huko mbele hujui kuna nini utaishi kwa amani kuliko kuwaza kuna maisha mengine mbeleni. Mambo kama roho, malaika, mbingu, moto, pepo ni ngano za kumfanya mwanadamu awe na utulivu na amani tu duniani.

Wanasema wataalamu wa “BIG THINK” kwamba hakuna kitu baada ya kifo, hakuna. Mfano, ukiambiwa hebu fikiria umekufa unaona nini? Wengi husema wanaona ndugu zao wanalia na wako kwenye jeneza. Ila ukweli ni kwamba unachosema sio unachoona, bali ni unachojua kwani unaona kila siku watu wakifa hali inakuwaje. Hivyo basi, kama huwezi kuona inakuwaje ukifa, basi hakuna maisha baada ya kifo, inaelezwa.

Historia inadai hata wayahudi wa zamani, kabla ya kuzaliwa Yesu, waliamini ukifa umekufa, hakuna nafasi nyingine ya maisha. Kila dini ina Mungu wake, na kila mtu anaamini dini yake ni ya kweli zaidi, na wengi dini zao wamerithi bila kuhoji, kuna hatari kwamba unachoamini kinaweza kisiwe cha kweli, na siku ukigundua, utajua umepoteza muda kubeba hofu maisha yako yote.

Wachambuzi wa Biblia wanasema kwenye agano la kale, hakuna sehemu ambapo panaonesha dhahiri kuwa kutakuwa na maisha baada ya kifo. Na dhana ya uzima wa milele haina maana utaishi milele baada ya kufa, bali wayahudi waliamini ukiishi na watu vizuri utaishi milele, mioyoni mwao.

Swali, kuna faida gani kuishi miaka 80, kama utafufuliwa tena? Ili ufanye nini? Iweje, upate nini? Kwani ukifa au ukiwa hai, unamuongezea au kumpunguzia nini Mungu anayemuamini? Kuna kitu anapata au anakosa kwako?

error: Content is protected !!