Tanzania yapanda nafasi 3 viwango vya FIFA

HomeMichezo

Tanzania yapanda nafasi 3 viwango vya FIFA

Tanzania imepanda kwa nafasi tatu katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Septemba

Kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotangazwa leo, Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 135 hadi ya 132 na kuzipiku nchi za Togo, Lithuania na Comoro ambazo zilikuwa juu yake katika viwango vya ubora vya mwezi uliopita.

Ushindi dhidi ya Madagascar na sare iliyopata ilipocheza na DR Congo katika mechi za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mapema mwezi huu, unaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa Tanzania ifikishe jumla ya pointi 1115.37 ambazo ni ongezeko la pointi 21.61 kutoka zile 1093.76 ilizokuwa nazo mwezi uliopita

Hata hivyo licha ya kupanda kwa nafasi hizo, bado Tanzania inashika nafasi ya tano kwa upande wa nchi zinazounda Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) huku ikiwa nafasi ya 37 kwa Afrika.

error: Content is protected !!