Mwenyekiti wa Kitongoji aua mkewe na kujinyonga

HomeKitaifa

Mwenyekiti wa Kitongoji aua mkewe na kujinyonga

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Urua chini kijiji cha Mfuruashe wilayani Rombo, Augustine Moshi mwenye umri wa miaka 35 amemuua mkewe Anastazia Augustine mwenye umri wa miaka 31 kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na yeye kujiua kwa kujinyonga.
 
Kabla ya tukio hilo kutendeka familia hiyo inadaiwa kuwa ilikuwa na migogoro kwa takribani mwezi mmoja uliopelekea Anastazia kwenda kuishi kwa wazazi wa mume wake baada ya kupigwa na mumewe. Wazazi wa mwanaume waliamua kusuluhisha ugomvi huo kwa kuwashirikisha wazee. Siku moja baada ya kusuluhishwa mwanaume huyo anadaiwa kumuingilia mkewe kinyume na maumbile hali iliyosababisha mwanamke huyo kwenda kushitaki kwa wazazi ndipo wazazi wakaa chini na kusuluhisha.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia uliosababishwa na wivu wa kimapenzi. “Upelelezi bado unaendelea miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Huruma. “Kwa mazingira ya tukio hili natoa wito kwa jamii kutambua matatizo yetu katika familia ili kutafuta njia madhubuti zitakazoweza kutatua migogoro vilevile kwa wanandoa au watu waliopo kwenye mahusiano ya kimapenzi wahakikishe wanapata watu sahihi ndani ya familia ili kuweza kuwatatulia migogoro yao kuepuka mauji kama hayo yaliotokea”, alisema Kamanda wa Polisi
error: Content is protected !!