Apigwa na kufariki akimgombania mhudumu Bar

HomeKimataifa

Apigwa na kufariki akimgombania mhudumu Bar

Kijana mmoja David Andega (24), kutoka kaunti ya Homa nchini Kenya amefariki duniani baada ya kupigwa na jiwe kichwani wakati akipigana kisa mhudumu wa baa anayesemekana kuwa mpenzi wake.

Andega alienda kwenye baa anayofanyia kazi mpenzi wake akiwa na rafiki yake, na walipofika hapo walimkuta mwanamke huyo akiwa na mwanaume mwingine na baada ya kijana huyo kuwaona akina Andega alikimbia na ndipo wakanza kumfukuzia na pikipiki.

Baada ya kumkamata na kuanza kumpiga, mwanaume huyo alichukua jiwe na kumpiga Andega kichwani na ndipo alianguka chini na kupoteza fahamu, mwanaume huyo alipoona Andega amepoteza fahamu alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Rafiki aliyekuwa na Andega aliita watu wamsaidie kumpeleka hospitali na walipofika daktari aliwapata taarifa kwamba tayari ameshafariki, mwili wa Andega umehifadhiwa mochwari huku polisi wakimshikilia yule msichana ambaye ni muhudumu wa bar kwa maelezo zaidi.

error: Content is protected !!