Tanzania yarejesha magari 20 yaliyoibwa Kenya

HomeKimataifa

Tanzania yarejesha magari 20 yaliyoibwa Kenya

Mkuu wa Wilaya ya Loitokitok nchini Kenya, Wesley Koech ameishukuru na kuipongeza serikali ya Tanzania kufanikisha kukamata na kurejesha magari 20 na pikipiki zilizoibwa nchini humi.

Koech alisema hayo mjini Loitokitok, Kenya katikak kikao cha ujirani mwema kati ya Wilaya hiyo na Wilaya ya Rombo, Tanzania. Koech alisema Serikali ya Kenya imeimarisha uhusiano wa ujirani mwema na Tanzania na wataimarisha uhusiano na wananchi wa Rombo.

Mkuu wa Wilaya ya Taveta, nchini Kenya, Joseph maina alisema Tanzania inastahili pongezi kwa kuwasamehe na kuwaachia huru maofisa polisi wa Kenya waliongia nchini wakiwa wamebeba silaha za moto.Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamisi Maigwa alisema serikali ya Tanzania imejipanga kuondoa kero na vikwazo vinavyoathiri ujirani  mwema katika ya Rombo Loitokitok.

error: Content is protected !!