Breaking: Mwafrika wa kwanza atunukiwa ‘Uprofesa’ chuo kikuu Oxford baada ya miaka 925 ya chuo hicho

HomeKimataifa

Breaking: Mwafrika wa kwanza atunukiwa ‘Uprofesa’ chuo kikuu Oxford baada ya miaka 925 ya chuo hicho

Patricia Kingori, ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya kiafrika (mweusi) kupata cheo cha kitaaluma cha uprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Oxford katika miaka 925 tangu chuo hicho kianzishwe.

Particia pia anashikilia rekodi nyingine kwa kuwa Profesa mdogo zaidi kuwahi kutokea kwenye asili ya Afrika kwenye chuo cha Oxford. Ameandika Profesa Patricia akishukuru, “Kwa kazi yangu kutambulika ni heshima kubwa sana kwangu, nashukuru na pia ningependa kuwashukuru watu watu wote walionipa moyo na kuniunga mkono katika safari yangu”..

Kwa mujibu wa Somerville, jarida la mtandaoni la chuo cha Oxford, Profesa Patricia Kingori ni Mwingereza mwenye asili ya Kenya ambaye ni mwana taaluma kutoka chuo cha kitivo cha Ethox Centre kinachohusika na masuala ya tafiti za maadili nchini Uingereza chenye lengo la kuboresha maadili hasa katika mazingira ya sehemu za afya.

Kingori alizaliwa Kenya, lakini alihamia eneo la Saint Kitts huko visiwa vya Karibiani akiwa mtoto bado, aliishi huko hadi alipofika umri kati ya miaka 10 – 15 ndio alipohamia London Uingereza.

Kingori anashaha ya Sosholojia kutoka Royal Holloway katika Chuo Kikuu cha London na baadae akahudumu kama mtafiti msaidizi katika taasisi hiyo. Kingori mara nyingi alijikita utafiti wake ulijikita hasa katika kuangazia changamoto za wafanyakazi katika sekta ya afya.

Kingozi pia aliwahi kuwa mshauri katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO), Save the Children, Medicins San Frontieres na mengineyo.

error: Content is protected !!