Omicron yaingia Rwanda, 6 waambukizwa

HomeKimataifa

Omicron yaingia Rwanda, 6 waambukizwa

Waziri ya Afya nchini Rwanda Daniel Ngamije imethibitisha kuwepo kwa watu 6 waliokutwa na Virusi vya corona aina ya Omicron jana na kusema kwamba kirusi hicho kinaenea kwa kasi licha ya kuwa serikali imeshaanza kuchukua tahadhari namna ya kuthibiti kuenea kwa kirusi hicho.

“Baraza la mawaziri tayari wamesitisha shughuli za vilabu vya usiku na burudani ya bendi ya moja kwa moja na pia ifahamike kwamba wageni wote wa nje wanaofika nhcini lazima wawekwe karantini kwa masaa 24 katika hoteli iliyoteuliwa kwa gharama zao wenyewe,” amesema Ngamije.

Takwimu zinaonyesha kwamba Rwanda ina zaidi ya watu 101,000 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na vifo 1,344 tangu kuanza kwa ugonjwa huo Machi mwaka jana.

error: Content is protected !!