Ashikiliwa kwa kubaka watoto watatu

HomeKitaifa

Ashikiliwa kwa kubaka watoto watatu

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia kijana mmoja mkazi wa Nshambya, Bukoba kwa tuhuma ya kuwabaka watoto watatu wa darasa la tatu na nne, wenye umri kati ya miaka 10 na 12

Michael Martini (30) alitekeleza ukatili huo Februari mwaka huu katika msitu wa Serikali wa Rwendimi kata ya Ijuganyondo Manispaa ya Bukoba watoto hao walipoenda kuchanja kuni.

Kaimu  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Maketi Msangi amesema mtuhumiwa aliwavizia watoto hao akawakamata na kuwatishia kuwakata kwa panga kama watapiga kelele na kisha kuwabaka.

Ameongeza kuwa “Mara baada ya kufanya kitendo hicho cha kikatili mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana kuogopa kukamatwa hata hivyo watoto hao walimtambua kwa sura mtuhumiwa huyo.”

Msako wa jesi la polisi kumtafuta mtuhumiwa ulifanikiwa Mei 24, 2022 majira ya jioni walipomkamata mtuhumiwa katika kijiji cha Kyansozi kata ya Maruku, Bukoba Vijijini.

Mtuhumiwa atapandishwa kizimbani mara baada ya upelelezi kukamilika.

error: Content is protected !!