Kesi ya Lissu yashindwa kuendelea, mashahidi wapo nje ya nchi

HomeKitaifa

Kesi ya Lissu yashindwa kuendelea, mashahidi wapo nje ya nchi

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu imeshindwa kuendelea leo leo Jumatano kutokana na mashahidi watatu wa mshtakiwa kushindwa kufika mahakamani, ikitajwa kuwa wapo nje ya nchi.

Mashahidi hao ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda; Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGPCamilius Wambura; pamoja na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan King’ai.

Akiongea baada ya mahakama kurejea mchana huu, Lissu amesema baada ya kuzungumza na msajili wa Mahakama, ameambiwa kuwa mashahidi wote watatu walipelekewa barua za wito Dodoma, lakini wote watatu wanasemekana wapo nje ya nchi na hivyo wameshindwa kuitikia wito huo.

Kwa mujibu wa Lissu, msajili amesema kati yao, shahidi mmoja ambaye ni DCI Ramadhan Kingai, anatazamiwa kurudi nchini leo na msajili amemuahidi siku ya Ijumaa, Kingai atakuwepo mahakamani ili kuitikia wito huo wa Mahakama.

Wengine wawili, CDF Mkunda na IGP Wambura haijulikani watarudi lini. Katika mazingira hayo, Lissu ameiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi siku ya Ijumaa, akisema asubuhi atakutana na kushuriana na shahidi huyo mchana, saa nane na nusu ili asubuhi aitumie kushuriana na huyo shahidi aliyeambiwa atakuja.

 

error: Content is protected !!