Polisi watano na mahabusu saba wafariki kwenye ajali Singida

HomeKitaifa

Polisi watano na mahabusu saba wafariki kwenye ajali Singida

Askari polisi watano na mahabusu saba wamefariki katika ajali iliyotokea eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba, Singida leo majira ya saa 1:30 asubuhi baada ya lori la mafuta lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Rwanda kugongana uso kwa uso na gari la Polisi.

Ajali hiyo imetokea wakati polisi walipokuwa wakiwasafirisha mahabusu kutoka Kituo cha Polisi Shelui, Iramba, kwenda Mahakama ya Wilaya ya Kiomboi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani.

Wengine wawili, ambao ni dereva wa lori la mafuta na askari mmoja, wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema uchunguzi wa awali umeonesha chanzo ni kufeli kwa breki za lori hilo.

error: Content is protected !!