Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekusanya TZS bilioni 150.04 kupitia tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere (Kigamboni) katika kipindi cha miaka 10 tangu daraja hilo lilipoanza kutumika Mei 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema mradi huo uligharimu TZS bilioni 345.20, ikiwemo TZS bilioni 328.74 za ujenzi na TZS bilioni 16.46 za fidia kwa wananchi waliohamishwa kupisha mradi.
Amesema daraja hilo lilipangwa kurejesha fedha za uwekezaji ndani ya miaka 30, na kufikia Juni 2026 tayari NSSF ilikuwa imekusanya TZS bilioni 150.04 kutokana na tozo za watumiaji.
Katika kipindi hicho, NSSF pia ilitumia TZS bilioni 25.81 kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo ya daraja hilo.


