Polisi wawili washikiliwa kwa kumfanyia vitendo vya kingono mtoto Kenya

HomeKitaifa

Polisi wawili washikiliwa kwa kumfanyia vitendo vya kingono mtoto Kenya

Askari polisi wawili wa kituo cha doria cha Kinjo, Kaunti ya Meru nchini Kenya, wamekamatwa kwa tuhuma za kumfanyia vitendo vya  kingono mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na nusu katika nyumba za makazi ya polisi.

Tukio hilo liliripotiwa na mama wa mtoto huyo baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa katika hali mbaya jioni ya Oktoba 9, 2026, alipokuwa akicheza nje.

Uchunguzi wa kitabibu uliofanyika katika Hospitali ya Nairobi Women’s, tawi la Meru, umebaini majeraha yaliyohusishwa na madai ya ukatili huo. Askari hao, wametajwa kuwa ni Nicholas Njagi na James Mutabari.

Aidha, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imepewa siku 14 za kuwashikilia kwa ajili ya uchunguzi kabla ya kusomewa mashtaka rasmi.

error: Content is protected !!