Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na maafisa wake wameshinda Tuzo ya Haki za Binadamu ya Sakharov 2026, ambayo hutolewa na Bunge la Ulaya kwa mtu au taasisi iliyoongoza katika kutetea haki za binadamu na uhuru wa mawazo.
Tuzo hiyo imetolewa ikiwa ni chini ya wiki mbili tangu aliyekuwa Jaji wa ICC, Navi Pillay, kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel.
ICC imesema tuzo hiyo imetolewa wakati mahakama hiyo na maafisa wake wanakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa, ikiwemo vikwazo vinavyolenga kuathiri utekelezaji wa majukumu yake ya kimahakama.
Washindani wengine wa tuzo hiyo walikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na ndugu wawili kutoka Iran, Taraneh na Romina Rahimi.


