Wanne wafikishwa mahakamani tuhuma za kumshambulia polisi

HomeKitaifa

Wanne wafikishwa mahakamani tuhuma za kumshambulia polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewafikisha mahakamani watu wanne wakikabiliwa na mashtaka manne ya jinai, likiwemo la kumshambulia askari Polisi, kukaidi amri halali, kumzuia askari Polisi kutekeleza wajibu wake na kuharibu mali kwa makusudi.

Washtakiwa hao ni Baraka Mapunda (34), mkazi wa Mwanza, Goodluck Simbachawene (33), mkazi wa Dar es Salaam, Steven Makungu (33), mkazi wa Mwanza, pamoja na Willy Wandola, mkazi wa Shinyanga.

Imeelezwa kuwa, mnamo Oktoba 17, 2026, katika eneo la Nyamanoro, Wilaya ya Ilemela, washtakiwa walimshambulia askari polisi, Issa Ibrahim Issa kwa kumkaba shingoni na kumpiga ngumi ya kifua na hivyo kumsababishia madhara mwilini kinyume na Kifungu cha 241 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 Toleo la 2023.

Akiendelea kusoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali ameeleza kuwa, shtaka la pili linawakabili washtakiwa wote wanne, ambapo inadaiwa kuwa, mnamo Oktoba 17, 2026, katika eneo la Ghana, Wilaya ya Ilemela, kwa pamoja walikaidi amri halali iliyotolewa na Sajenti wa Polisi Jackline, aliyewezeshwa kisheria kutoa amri hiyo.

error: Content is protected !!