Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuna mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi, karibu na visiwa vya Ushelisheli, takribani kilomita 1,600 kutoka Pwani ya Tanzania, ambao unatarajiwa kuimarika na kuwa kimbunga ndani ya siku nne zijazo.
Kwa mujibu wa TMA, mgandamizo huo unaelekea katika Pwani ya Tanzania na unaweza kuimarisha mifumo inayosababisha mvua katika maeneo ya ukanda wa Pwani na maeneo jirani, hususan kuanzia Oktoba 24, 2026.
Kutokana na hali hiyo, TMA imewataka watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hiyo, pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa sekta husika.
TMA imesema inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini, na itaendelea kutoa taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.


