Ndejembi ataka wanawake kupewa nafasi katika utatuzi wa migogoro

HomeKitaifa

Ndejembi ataka wanawake kupewa nafasi katika utatuzi wa migogoro

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, amezitaka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kuwapa wanawake nafasi yenye ushawishi katika maamuzi, mazungumzo ya amani na utatuzi wa migogoro, huku akisisitiza maazimio yaambatane na hatua zinazotekelezeka na kupimika.

Ametoa wito huo alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, kufungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Wabunge Wanawake wa Ukanda wa Maziwa Makuu, unaofanyika Novemba 2 hadi 5, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.

Ndejembi amesema wanawake ni viongozi, wapatanishi na wajenzi wa amani, hivyo ni muhimu kuondoa mila kandamizi, ubaguzi na vikwazo vya kiuchumi vinavyopunguza ushiriki wao.

Aidha, amesisitiza kuwa Tanzania inaendelea kuwawezesha wanawake kupitia fursa za uongozi, elimu, masoko, mitaji na mikopo yenye masharti nafuu.

 

error: Content is protected !!