Achinjwa hadi kufa kwa kuolewa bila ridhaa ya wazazi

HomeKimataifa

Achinjwa hadi kufa kwa kuolewa bila ridhaa ya wazazi

Mwanamke mmoja, umri miaka 19 huko nchini India katika eneo la Aurangabad amevamiwa na kuchinjwa na kaka zake wawili baada ya kutoroshwa na kuolewa na mwanaume ambaye hawakumtaka.

Awali familia ya msichana huyo ilimkataa mwanaume wa msichana huyo kutokana na umasikini wake. Msichana aliamua kutoroka nyumbani kwao na kutumkia kwa mwanaume wake, kitendo kilichowasirisha sana ndugu zake.

Tangu msichana huyo alimkie kwa mwanaume wake, alikuwa na mawasiliano madogo sana na familia yake. Lakini licha ya kuwakera wazazi wake kwa kitendo alichofanya, bado Mama yake mzazi hakusita kumtembelea nyumbani kwake kila mwisho wa juma.

Kabla ya kukatwa kichwa kikatili na kaka yake, alikuwa jikoni akiandaa chai kwa ajili ya mama na kaka yake, ndipo alipovamiwa kwa nyuma na kaka yake na kukatwa kichwa huku mama yake akitazama. Kitendo kinachosikitisha zaidi ni kwamba mwanamke huyo alikua mjamzito wakati anatendewa unyama huo.

Wanaharakati nchini India wanasema kuwa mamia ya wasichana huuwawa kila mwaka nchini humo kwa kosa la kuolewa na wanaume ambao hawajapewa ridhaa za wazazi wao. Machi mwaka huu polisi katika jimbo la Uttah walimkamata mwanaume aliyemchinja bintiye kwa madai ya binti huyo kuolewa na mwanaume ambaye Baba yake hakumridhia.

error: Content is protected !!