Wafanyakazi 900 wafukuzwa kazi muda mmoja kupitia ‘Zoom Call’

HomeKimataifa

Wafanyakazi 900 wafukuzwa kazi muda mmoja kupitia ‘Zoom Call’

“Kama umepokea simu hii muda huu, wewe ni mmoja ya watu waliofukuzwa kazi”, aliongea Vishal Garg, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kupangisha na kuuza majengo inayojulikana kama Better.com. Katika simu hiyo moja tu, wamefukuzwa wafanyakazi 900 kwa muda mmoja.

Bosi huyo aliwapigia simu wafanyakazi wake kupitia mtandao wa Zoom. Baadi ya maoni katika mtandao wa kijamii wamesema kuwa kitendo hiko kilikuwa ni cha kinyama na kibaya sana kwa kiongozi wa taasisi kuwafanyia wafanyakazi wake hasa katika wakati huu ambao watu wanaelekea kwenye Sikukuu ya Krismasi.

Garg amesema kuwa kuwa ufanisi, mapato pamoja na masoko ni moja ya sababu kubwa nyuma ya kufuza hiyo kubwa ndani ya kampuni hiyo.

Simu ya bosi ilikuwa kama ifuatavyo

“Habari zenu, nashukuru kwa kujiunga na simu hii, lakini sina habari nzuri kwenu. Soko limebadilika, kama mjuavyo ni lazima tufanye maamuzi magumu kwenye nyakati ngumu ili tuweze kujinusuru na tufikie malengo yetu.

“Huu sio ujumbe ambao mngependa kuusikia, lakini mwisho wa siku ni uamuzi wangu na ningependa ufuatwe. Ni mara ya pili katika maisha yangu kufanya kitendo kama hiki, na mara ya kwanza nililia sana. Sasa habari ni kwamba tunapunguza 15% ya wafanyakazi wetu kwa sababu za masoko, ufanisi, biashara pamoja na mapato, kama upo kwenye simu hii bado jua umefukuzwa kazi, na tangazo hili linaanza mara moja”.

Wafanyakazi hao wamenukuliwa na kituo cha runinga cha BBC wakilalamika na kusema kuwa bosi huyo hakutenda vyema kabisa, kwani hata kama alilazimika kuwasimamisha kazi, alipaswa kutumia utaratibu mwingine nasi huo aliotumia.

 

error: Content is protected !!