Vijana waitwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea ya JKT

HomeKitaifa

Vijana waitwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea ya JKT

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa wito wa Vijana wa Kitanzania kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2026/27.

Akitoa Taarifa kwa Umma Novemba 12, 2026 Makao Makuu ya JKT Chamwino, Dodoma kwa niaba ya Mkuu huyo wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema nafasi hizo zimetolewa kwa vijana wa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, wanaokidhi vigezo na sifa zilizoainishwa.

Brigedia Jenerali Mabena ameongeza kuwa usaili wa kujiunga na mafunzo hayo utaanza Novemba 16, mwaka huu, ambapo vijana watakaoteuliwa kujiunga na mafunzo watatakiwa kuripoti makambini kuanzia Desemba 10, 2026 hadi Desemba 15, 2026.

Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amefafanua kuwa JKT haitoi ajira na halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya Ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya kiserikali, bali hutoa mafunzo yatakayosaidia vijana kujiajiri mara baada ya kumaliza mkataba wao na JKT.

error: Content is protected !!