Kenya yasema haina tena wagonjwa wa Ebola

HomeKimataifa

Kenya yasema haina tena wagonjwa wa Ebola

Kenya imetangaza kuwa haina tena wagonjwa wa Ebola baada ya Wizara ya Afya kusema kuwa wagonjwa wote saba waliothibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Waziri wa Afya, Aden Duale, amesema wagonjwa watano waliruhusiwa kutoka hospitalini Novemba 3, mwingine Novemba 6, huku mgonjwa wa mwisho akiruhusiwa Jumatano.

Ameongeza kuwa watu wote 135 waliokuwa wamekutana na mgonjwa aliyeingiza ugonjwa huo nchini humo wamekamilisha ufuatiliaji wa afya na kuachiwa kutoka vituo vya karantini.

Hata hivyo, serikali imesema itaendelea kuchunguza afya za wasafiri katika maeneo yote 26 ya kuingilia nchini humo. Hadi sasa, zaidi ya wasafiri 760,000 wamepimwa katika maeneo hayo.

Ebola iligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Kenya Oktoba 3, 2026 ikiripoti jumla ya maambukizi tisa na vifo viwili vilivyohusishwa na ugonjwa huo.

 

 

error: Content is protected !!