Rais Samia awaasa vijana kulinda amani ya nchi

HomeKitaifa

Rais Samia awaasa vijana kulinda amani ya nchi

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kulinda amani na usalama wa Tanzania wakati nchi ikijiandaa kupokea wageni wa kimataifa kwa ajili ya shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchini.

Rais Samia ametoa wito huo leo aliposalimia wananchi wa Bomang’ombe, wilayani Hai, akiwa njiani kuelekea mjini Moshi.

Amesema idadi ya watalii wanaoingia nchini na mikutano ya kimataifa inayofanyika Tanzania ni kielelezo cha nchi kuendelea kuwa salama. Pia ameitaja michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027, na mashindano ya urembo wa dunia mwaka 2027 kuwa miongoni mwa matukio yatakayoleta wageni wengi nchini.

Rais Dkt. Samia yupo mjini Moshi, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Shule ya Polisi mjini humo.

error: Content is protected !!