Rais Samia awasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu

HomeKitaifa

Rais Samia awasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Novemba 19, 2026 amewasili Mkoani Arusha kupitia Uwanja wa ndege wa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Akiwa Njiani kuelekea Ikulu ndogo Jijini Arusha, Mhe. Rais Samia alisimama na kuzungumza na wananchi wa Kibaoni, Ngaramtoni, Wilayani Arumeru.

Rais Samia pamoja na ratiba nyingine, Kesho Ijumaa anatarajiwa kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye shule ya Polisi Moshi Mkoani Kilimanjaro na Jumamosi Novemba 21, kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli, Mkoani Arusha

error: Content is protected !!