Ukiona dalili hizi, ujue anachepuka

HomeElimu

Ukiona dalili hizi, ujue anachepuka

Pengine unaona vitu ambavyo wewe unadhani kuwa ni tabia za kawaida tu, na kwamba huhitaji kuwa na mashaka, jiulize tena, kwani pengine kuna jambo linaendelea na wewe unakaa tu.

Hizi ni ishara sita ambazo huenda zikakudokeza kama mwenza wako anachepuka.

6. Kubadilika kitabia
Wengi hutumia kazi kama kisingizio, utaona anaanza kurudi nyumbani usiku au kwa kuchelewa na mara zote ukimuuliza atasema sababu ni kazi. Wengine huenda mbali na kubadili nywila za simu zao au barua pepe na kuficha taarifa zao za kifedha. Tabia yoyote ya usiri ni ishara kwamba mtu sio mwaminifu.

5. Kuwa na moods
Wakiishiwa visingizio, wataanza kutengeneza vipya. Hii inaweza kuwa kugombana kwa sababu ya kitu kidogo, na wengine hufikia hatua hata ya kuondoka nyumbani kwa saa kadhaa, ikiwa ni sababu tu ya kwenda kukaa na amtakaye.

4. Zawadi za kushtukiza
Kupewa zawadi sio vibaya, lakini kuna wakati inashtusha hasa kama sio tabia yake kufanya hivyo, mara anaanza kuleta zawadi nyingine, basi huenda kuna kitu kinamuumiza ndani na hivyo ni njia yake ya kusuluhisha.

3. Anatumia sana mitandao ya kijamii
Kama muda mwingi yupo Facebook au Twitter au Whatsapp, huenda huko ndipo mchepuko wake alipo. Lakini kabla hujafanya maamuzi, ni vyema ukatafuta ukweli kwanza.

2. Hatengi muda kwa ajili yako na mtoto
Kama kila mkipanga kitu anatafuta sababu ya kutokuwepo, au hatengi muda kwa ajili ya familia kama ilivyokuwa awali, basi huenda ni ishara kwamba ana “kidumu” nje. Hii huenda ikachangiwa kuwa anashindwa kuweza uzani sawa kati ya familia na mchepuko.

1. Mwonekano tofauti
Mwanzoni mwa uhusiano, wapenzi hupenda kuonekana nadhifu kila wanapotoka. Lakini muda unavyokwenda hili huweza kubailika. Ila ukiona mwenzako ameanza kuwa nadhifu kila mara akitoka mwenyewe, tofauti na mkitoka wote, huenda kuna kitu hakiko sawa.

Hizi ni dalili tu kuonesha kuwa kuna kitu kinaendelea, lakini haimaanishi kuwa uzionapo, ni lazima kiwepo, kikubwa ni kutenga muda kufuatilia kwa karibu ili kupata uhakika zaidi.

error: Content is protected !!