Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimemsimamisha kazi Rais wa chama hicho, Leah Ulaya kutokana na masuala mengi ikiwamo kushindwa kuwaunganisha walimu ma kushungulikia changamoto zao.
Kwa uamuzi huo Leah atasubiri hatma yake katika mkutano mkuu wa CWT utakaofanyika mwaka 2022. Katika kikao cha kumsimamisha kazi, kati ya kura zilizopigwa, 42 walitaka aendelee huku 131 wakitaka asimamishwe
Sababu zilizopelekea kiongozi huyo kusimamishwa ni:
1. Kushindwa kuwaunganisha walimu na kuelezea changamoto zinazowakabili
2. Kutoandaa mazingira ya uchaguzi wa katibu
3. Kunyofoa baadhi ya karatasi katika taarifa ya CAG
4. Kumwamuru katibu abatilishe uhamisho wa watumishi wanne kutoka makao makuu ya CWT kwenda wilayani
5. Kugoma kufanya ziara wakati fedha alichukua
Leah alichaguliwa Mei 2020 kushika wadhifa huo katika mkutano mkuu uliofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.