Sudan yazima jarabio la mapinduzi

HomeKimataifa

Sudan yazima jarabio la mapinduzi

Kumetokea jaribio la kuipindua serikali ya Sudan, lakini tayari limezimwa na jitihada za kurejesha hali ya utulivu zinaendelea.

Kituo cha Televisheni cha Taifa nchini humo kimeutangazia umma kuwa wapinge jaribio hilo, lakini hakikutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.

Mohammed Al Faki Suleiman, ambaye ni moja wa viongozi kutoka serikali ya kijeshi inayoongoza Sudan amesema kikundi cha waasi wenye silaha walikusudia kupindua serikali kwa kuanza kutaka kuweka vizuizini baadhi ya taasisi nyeti za Serikali. Hata hivyo hawakufanikiwa baada ya nia yao kubanika na kusimamishwa wakiwa ndani ya magari wakielekea kufanya hivyo.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa, wanajeshi wengi, wakiwemo wa ngazi za juu, wamewekwa chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba watatoa taarifa zaidi.

Kwa sasa taifa la Sudan liko chini ya Serikali ya mseto ambayo inajumuisha viongozi kutoka jeshini na wanasiasa ambao walichaguliwa watu.

error: Content is protected !!