Sote tu mashahidi kuwa Twitter ni moja kati ya mtandao wa kijamii ambao ni ngumu sana kupata wafuasi ukilinganisha na mitandao mingine. Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya masoko kidijitali, Gillsant (@Gillsalnt) ameeleza namna ambavo unaweza kupata wafuasi (followers) 1000 ndani ya mwezi mmoja (siku 30). Njia hizo ni kama zifuatazo.
- Kwanza kabisa fahamu malengo ya akaunti/ukurasa wako
Hii ni kujua kuwa unafungua ukurasa wa Twitter kwa malengo gani, unataka kufanya biashara, unataka kufanya siasa, unataka kujihusisha na michezo au jambo lolote lile, lakini ni lazima ujue unataka kufanya nini kama una malengo ya kukuza wafuasi. Ukiweza kufanya hivyo bila shaka utapata wafuasi wa namna yako, na kupitia hao ukurasa wako utakua. - Watu gani unawalenga
Lazima uwe na shabaha ya watu unaowataka. Ukiweza kujitofautisha, basi tofauti yako ndio itakayokuuza zaidi. Kama unauza nguo, basi mtu yeyote akiwaza kununua nguo au kujua maswala ya nguo basi jina lake limjie kwenye akili yake, kwa mtindo huo unaweza kukua, ila ni lazima uwe na shabaha kwanza.> Elimu ya biashara: Umuhimu wa matumizi sahihi ya muda katika kukuza biashara
- Tweet zako ziwahusu watu hao
Ukiwa unafanya michezo, basi tweets zako ziwe ni masuala ya michezo tu. Kama utachepuka kwenye mada nyingine basi iwe aghalabu au kwa uchache ili usipoteze utambulisho wako. - Fuata/Follow kurasa zinazoendana na maudhui yako
Hakikisha kuwa ‘una-follow’ akaunts/kurasa ambazo zina maudhui ya kufanana na yako. Njia hii ni rahisi kukuza uelewa wako juu ya jambo unalofanya, pili itakutengenezea itakuwa uwanda mpana wa kuandika na kutoishiwa maudhui kwenye jambo lako. - Tweet mara 3 kila siku, muda tofauti.
- Comment/Engage kwenye tweets za watu wengine, toa maoni, toa ushauri, saidia na hakikisha una comment vitu vya maana tu na mara nyingi kwenye accounts zenye followers wengi. Onesha upendo/like kwenye posts 30 kila siku.
- Follow account 67 kila siku