Rais Samia atuma salamu za pole Mtwara

HomeKitaifa

Rais Samia atuma salamu za pole Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu kufuatia ajali iliyotokea Mtwara na kusababisha vifo vya watu 10 wakiwemo wanafunzi nane vilivyosababishwa na ajali ya basi la shule.

Ajali hiyo imetokea leo Julai 26, 2022, baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Msingi ya King David kutumbukia shimoni katika eneo la Mjimwema, Mikindani, mkoani Mtwara.

Katika Salamu zake za pole alizoziandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema amesikitishwa na vifo hivyo na ametoa pole kwa wote waliopoteza jamaa zao. 

“Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na awajalie majeruhi wapone haraka,” amesema Rais Samia katika ukurasa wake.

error: Content is protected !!