Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 11 (Morata kuchukua nafasi ya Kane Tottenham, Adama Traore akinyatiwa na Liverpool)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 11 (Morata kuchukua nafasi ya Kane Tottenham, Adama Traore akinyatiwa na Liverpool)

Ralf Rangnick, aliyekuwa kocha wa klabu ya RB Leipzig ananyatiwa na Newcastle ili kuchukua nafasi ya ukurugenzi wa michezo (Telegraph).

Wamiliki wapya wa klabu ya Newcastle United wana mpango wa kumbadilisha kocha wa klabu hiyo huku wakihusishwa na Brendan Rodgers wa Leicester City. Pia kocha wa klabu ya Rangers Steven Gerrard na aliyekuwa kocha wa Borussia Dortmund Lucien Favre ni miongoni mwao wanaohusishwa na klabu hiyo (Mail).

Newcastle United itawasilisha ofa ya kuwasajili wachezaji wanne wa Manchester United katika dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari. Wachezaji hao ni mshambuliaji wa England Jesse Lingard (28), Anthony Martial (25), kiungo wa kati Donny van de Beek 24 na Beki Eric Bailly (Mirror).

Rafael Yuste, makamu wa rais wa klabu ya Barcelona amepuuza fursa ya klabu hiyo ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Haaland (21) msimu ujao (Mundo Deportivo – Spanish).

      > Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 10 (Pogba kutimkia Juventus, huku Newcastle ipo mbioni kumalizana na Steve Bruce)

Juventus itamtumia kiungo wake Aaron Ramsey (30) kama chambo cha kumvutia kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba (28) kurudi mjini Turin (Mail).

Mshambuliaji wa Brazil Neymar (29) amesema kwamba huenda kombe la Dunia la 2022 litakalofanyika nchini Qatar likawa lake la mwisho, kwa kuwa hana uhakika iwapo akili yake ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za soka (DAZN – Goal).

Kiungo wakati wa Italia Marco Verratti (28) anasema kwamba hana mpango wa kuondoka PSG na atahududumu kipindi chote kilichosalia katika klabu yake (France Info).

Barcelona ipo tayari kumuuza winga wake, Ousmane Dembele (24) iwapo mchezaji huyo mwenye hatoongeza mkataba nao na huenda klabu hiyo ya Uhispania ikaangalia uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling (26) kuchukua nafasi yake. (Sport – in Spanish)

Klabu ya Tottenham inamnyatia mshambuliaji wa Uhispania, Alvaro Morata (28) kama mbadada wa Harry Kane (28) anayetazamiwa kuondoka klabuni hapo. Morata ambaye kwa sasa yupo Juventus kwa mkopo kutoka Atketico Madrid (Fichajes).

Liverpool ipo tayari kuwasilisha ofa ya kumsajili winga wa Wolves Adama Traore, 25 (El Nacional)

Klabu ya Chelsea imepatia mkataba mpya kiungo wake, Andreas Christensen, makubaliano yapo hatua za mwisho kabla ya kutangazwa rasmi (Fabrizio Romano on Twitter).

 

error: Content is protected !!