Nchi maskini deni limeongezeka maradufu – Ripoti ya Benki ya Dunia

HomeKimataifa

Nchi maskini deni limeongezeka maradufu – Ripoti ya Benki ya Dunia

Ripoti ya takwimu za madeni ya mwaka 2022 inayotolewa na Benki ya Dunia inaeleza kuwa madeni ya nchi za kipato cha chini yameongezeka kwa asilimia 12 hadi kufikia dola bilioni 860 katika kipindi cha hadi mwaka 2020. Ripoti hiyo imetolewa Jumatatu (11/10/2021) katika Mkutano uliowakutanisha Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) Washington nchini Marekani.

               > Benki ya Dunia kushirikiana zaidi na Tanzania

Ripoti inaonesha kuwa deni hilo limekuwa zaidi kutokana na Mataifa hayo kuchukua fedha nyingi kutoka benki hiyo na kuzitumia kwenye vita dhidi ya UVIKO-19 katika mataifa yao.

Pia ripoti hiyo inaonesha kuwa mataifa ya kipato cha chini yalipewa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya pamoja na kuinua chumi zao zilizoathirika vibaya na janga la UVIKO-19. #clickhabari

error: Content is protected !!