Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 17 (Luka Jovic kutua Arsenal, huku Newcastle ikimnyatia Haaland)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 17 (Luka Jovic kutua Arsenal, huku Newcastle ikimnyatia Haaland)

Klabu ya Newcastle United inamsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, mchezaji huyo pia anafuatilwa na Real Madrid, Manchester City na Paris St-Germain (AS, via Sport Witness). Katika harakati za kuimarisha kikosi chao Newcastle imeamua ijitose kupata mshambuliaji anayejua kufunga na atakayeisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa.

Wakala wa Mohamed Salah amesafiri hadi Liverpool kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu mkataba mpya (Mirror, via Star Online). Salah ambaye kwa sasa anaonyesha kiwango kizuri ndani ya Anfield na kuisaidia timu yake kusalia kileleni mwa ligi kuu ya England ni mchezaji muhimu kwa Liverpool.

Manchester United imetenga pauni milini 70 kwa ajili ya dirisha lijalo la uhamisho, ambazo zitatumika ilimradi wanahisi kuwa wanaweza kupata taji la ligi kuu ya England (Star Sunday).

Mshambuliaji wa Real Madrid Mserbia Luka Jovic 23, amechaguliwa kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette 30, katika Arsenal (Fichajes). Lacazette anatarajiwa kuondoka Arsenal mwezi Januari baada kuonekana hana mafanikio kwa klabu hiyo, maamuzi ya Lacazette ni sahihi kutafuta klabu itakayomfaa kuendeleza kiwango na kipaji chake.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere 29, amemshauri beki wa England Declan Rice 22, akatae ofa za uhamisho kutoka Manchester United na Chelsea na aendelee kubakia West Ham (Mirror). Ushauri huu wa Wilshere anautoa kwa Rice yasije kumkuta yaliyomkuta yeye kupelekea kukosa timu ya kuchezea mpaka.

Wakala wa Robert Lewandowski (33) amethibitisha kuwa Manchester City ndio “timu anayoweza kuhamia” mshambuliaji huyo wa Bayern Munich mwenye (Bild, Star Online). Lewandoski kutokana na kiwango chake na uwezo alionao katika ufungaji wa magoli anastahili kuwepo Man City.

Kiungo wa kati wa Arsenal na nahodha wa Norway Martin Odegaard 22, yupo tayari kupokea wazo la kurejea Real Sociedad, aliyekuwa mlindalango wa Gunners Mat Ryan 29, anmesema hayo mchezaji huyo ambaye kwa sasa yupo Real Sociedad (Mundo Deportivo – Mirror Online).

Mlinzi wa klabu ya Sevilla Jules Kounde (22) amemuomba wakala wake kufanya mazungumzo na Manchester United, huku mchezaji huyo anawindwa na klabu za Chelsea na Real Madrid (El Nacional – Spanish).

Beki Dani Alves (38) aliyewahi kuichezea Barcelona amejitolea kujiunga tena na klabu hiyo kwa mkataba wa ‘garama ya chini’. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil sasa yuko huru baada ya kusitisha mkataba wake na Sao Paolo mwezi wa Septemba (AS Spanish). Uzoefu katika safu ya ulinzi ni muhimu Barcelona wanaweza kutumia nafasi hii kwa hayi ya uchumi wanayoipitia.

Liverpool wamejiunga katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Club Bruges Noa Lang (22) sambamba na Arsenal na Leeds (Calciomercato, via Teamtalk). Noa Lang huu ni muda way eye kuangalia timu itakayomfaa na itakayompa nafasi ya kucheza na kukuza kipaji chake kabla ya kuchua maamuzi yoyote ambayo anaweza kujutia baadae.

Kiungo wa kati wa Rangers Joe Aribo, 25, ananyatiwa na Crystal Palace (Football Insider). Ni moja ya hatua nzuri kwa Palace katika kuleta ushindani kwa wapinzani wake ligi kuu ya England.

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anasema pesa sio dhamana ya kufanikiwa na atashangaa Newcastle ikichukua taji la Ligi Kuu kabla ya 2030 (Telegraph). Kuchukua mataji inapasa kuwa na kocha mwenye mbinu za kuibeba timu na kuifikisha inapohitajika sambamba na wachezaji makini watakaojitolea kwa ajili ya timu.

error: Content is protected !!