Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 18 (Bale mbioni kutua Arsenal Januari, Ansu Fati ngoma ngumu ndani ya Barcelona)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 18 (Bale mbioni kutua Arsenal Januari, Ansu Fati ngoma ngumu ndani ya Barcelona)

Aliyekuwa kiungo wa Chelsea na England Ross Barkley 27, anawaniwa na klabu ya Burnley dirisha dogo la usajili mwezi Januari (Sun). Kutokana na kiwango chake anachokionesha Burnley awamevutiwa kupata huduma ya kiungo huyo.

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale 32, atapokea ofa ya usajili kutoka Arsenal ifikapo dirisha dogo la usajili mwezi Januari (Defensa Central – Spanish). Arsenal wanahitaji kuimarisha kikosi chao chini ya Mikel Arteta anayeaminiwa kuifikisha klabu hiyo katika mafanikio.

Barcelona haitamshawishi Paul Pogba wa Manchester United wakati mkataba wa kiungo huyo utakapokwisha mwisho wa msimu kwa kuwa klabu hiyo ya Hispania haitaweza kumudu mshahara wa nyota huyo mwenye miaka 28 (AS). Barcelona imekuwa ikisua sua kichumi hivi karibuni kupelekea kuachwa Lionel Messi, hii ni wazi kwamba hawatamudu mshahara wake.

  > Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 17 (Luka Jovic kutua Arsenal, huku Newcastle ikimnyatia Haaland)

Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Michael Edwards anawaniwa na Real Madrid ili kuisaidia klabu hiyo ya Hispania kwenye masuala ya uhamisho wa wachezaji (Sun).

Wakala Matthijs de Ligt 22, Mino Raiola amezungumza na klabu za Manchester City na Chelsea kwa matumaini ya kuchagiza uhamisho wa mlinzi huyo wa kati (Calciomercato – Italian). De Ligt amekuwa akiwaniwa sana na Chelsea kuboresha safu yao ya ulizni iwapo Antonio Rudiger ataondoka.

Aston Villa imemuweka katika orodha ya wachezaji inayowataka beki wa kushoto wa Bologna Aaron Hickey 19, baada ya kuonyesha kiwango bora Serie A, lakini beki huyo hana haraka ya kuondoka Italia (Sun).

Mazungumzo ya mkataba mpya wa shambuliaji wa Barcelona na Hispania Ansu Fati (18) yamekwama baada ya wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes kutaka mchezaji wake apewe mkataba wa miaka na kukataa kuwekwa kwa kipengele cha mkataba kinachomfunga mchezaji huyo kwa thamani ya £844m (El Nacional – in Catalan). Hii inakuja kutokana na kiwango alichonacho mchezaji huyo akiwa uwanjani.

Klabu za Tottenham Hotspur na Newcastle United zinamuania mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, 21 (Sun). Ni mchezaji anayeweza kusaidia timu yake inapozidiwa kupelekea kwa timu hizi kuhitaji huduma yake.

error: Content is protected !!