Vurugu za Machinga Kariakoo, Mkuu wa Mkoa DSM atoa neno

HomeKitaifa

Vurugu za Machinga Kariakoo, Mkuu wa Mkoa DSM atoa neno

Video mbalimbali zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikionesha vurugu katika eneo la Kariakoo kati ya Jeshi la Polisi na wafanyabiashara wadogo (Maching) katika eneo la Msimbazi Kariakoo.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amesema kuwa, taftrani hiyo imetokea wakati viongozi wa wamachinga wakiunga mkono jitihada za Serikali katika kuwapanga vizuri wamachinga na kuwatoa wengine ambao wameziba njia za watembea kwa miguu.

    > Kauli ya RC Makalla siku 3 kabla ya zoezi la kuondoa machinga

RC Makalla ametoa pongezi za dhati kwa viongozi wa wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema kuwa licha baadhi ya wamachinga kuonesha kupinga maagizo, lakini viongozi waliendelea kufanya kazi yao.

Makala  amewatia moyo viongozi wa wamachinga kuendelea kufanya kazi na kwa kuonesha ukomavu katika kutekeleza maagizo ya Serikali na pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufika haraka eneo la tukio na kutoa ulinzi wa kutosha kwa viongozi wa wamachinga wakati wakitekeleza wajibu wao.

error: Content is protected !!