Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 23 (Sanchez kutimkia Everton, huku Real Madrid ikimfuatilia Antonio Rudiger)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 23 (Sanchez kutimkia Everton, huku Real Madrid ikimfuatilia Antonio Rudiger)

Kipaumbele cha Antonio Rudiger ni kubakia Chelsea, lakini mchuano wa kutaka saini yake ‘uko wazi’ (Fabrizio Romano).

Klabu ya Everton inajiandaa kufanya uhamisho wa mshambuliaji wa Inter Milan na Chile Alexis Sanchez 32, huku mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Arsenal na Manchester United akiwa huru kuondoka katika klabu ya Italia mwezi wa Januari (InterLive – in Italian).

Chelsea haitatekeleza azimio lake la awali la kusaini mkataba wa kudumu wa pauni milioni 34 na kiungo wa kati wa Atletico Madrid, Saul Niguez (26). Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alihangaika kupata mafanikio ya kimchezo tangu alipojiunga na the Blues kwa mkopo mwezi Agosti (La Razon – Spanish).

Real Madrid Bayern Munich wanaamini kabisa kuwa watasaini mkataba na kiungo Mjerumani Antonio Rudiger 28, ambaye mazungumzo kuhusu mkataba wake na Chelsea bado yapo njia panda (ESPN).

    > Tetesi za Soka Ulaya Oktoba 22, 2021

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek 24, amemuomba wakala wake kuangalia uhamisho wake wa kuhamia Real Madrid (Sun).

Chris Smalling 31, anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka Roma, mwezi wa Julai (Calciomercato – Italian).

Mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo 36, ‘aliharibiwa’ na ‘kuvunja sheria za usawa na unyenyekevu’ akiwa Juventus (Mail).

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta atakataa ofa yoyote ya kumuuza mshamuliaji Alexandre Lacazette, 30, mwezi Januari na badala yake atamruhusu kuondoka huru mkataba wake utakapoisha msimu ujao (Sun).

Klabu za Manchester City, Tottenham, Liverpool na Newcastle zinamtaka winga Ousmane Dembele, 24, ambaye ana uwezekano wa kuondoka Barcelona msimu ujao (90Min).

error: Content is protected !!