Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 22 (Fonsesca njiani kuchukua nafasi ya Steve Bruce, Van de Beek kuikacha Man United Januari)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 22 (Fonsesca njiani kuchukua nafasi ya Steve Bruce, Van de Beek kuikacha Man United Januari)

Klabu ya Newcastle imeanza mazungumzo na Paulo Fonsesca kuchukua nafasi ya kocha Steve Bruce aliachia nafasi hiyo hivi karibuni, mazungumzo hayo yataendelea leo kati yake na bodi ya Newcastle – makubaliano yanakaribia juu ya mkataba wa muda mrefu. Fonseca alijiandaa kukubali ikiwa bodi ya Newcastle itawasha ‘taa ya kijani’ (Fabrizio Romano).

Kiungo wa zamami wa Arsenal na England Jack Wilshere, 29, yuko tayari kuhamia ligi kuu ya Marekani kujiunga na klabu ya Inter Miami (Talksport).

Barcelona ipo mbioni kuipiku Real Madrid katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao (AS – in Spanish).

> Tetesi za Soka Ulaya Oktoba 21, 2021 (Tielemans mbioni kuikacha Leicester City, huku Dyabala mambo safi ndani ya Juventus)

Kiungo wa Manchester United Donny van de Beek 24, hatarudi Ajax lakini kuna nafasi kubwa kwamba ataondoka Old Trafford mwezi januari (Fabrizio Romano).

Beki wa Juventus Giorgio Chiellini anasema ingekuwa bora mshambuliaji wa Ureno wa Cristiano Ronaldo 36, kuondoka Juve na kujiunga na Manchester United mapema zaidi (DAZN, via Goal).

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema klabu hiyo haijapokea ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wake wa Uholanzi Van de Beek, licha ya uwepo wa tetesi nyingi (RTL7, via Manchester Evening News).

Klabu za Liverpool, Manchester United na PSG walimpa ofa ya pesa nyingi Ansu Fati (18) ili ajiunge nazo kabla ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kusaini mkataba mpya Barcelona (Cope).

error: Content is protected !!