TAHADHARI: Mlipuko wa Kipindupindu

HomeKitaifa

TAHADHARI: Mlipuko wa Kipindupindu

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametahadharisha kuwapo mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika baadhi ya mikoa na kuwataka Watanzania kuzingatia usafi wa mazingira, maji na chakula, ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko.

Ummy aliyasema hayo jana mkoani Dar es Salaam , wakati wa uzinduzi wa semina ya mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kuijengea uwezo serikali na wadau mbalimbali katika kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

“Tanzania kuna jumla ya wagonjwa 519 wenye ugonjwa wa kipindupindu kati yao 11 wameshafariki dunia, gonjwa hili limeshamiri zaidi katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi kuanzia Agosti 3 hadi 27 mwaka huu,” alisema na kuongeza:

“Wamegundulika wagonjwa 39 kutoka Mkoa wa Katavi Wilaya ya Tanganyika kwa hiyo kipekee tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza fedha nyingi na nguvu kubwa katika upatikanaji wa majisafi na salama katika maeneo mbalimbali.”

Aidha, aliwaagiza wakuu wa wilaya nchini kuweka vipaumbele kwenye kudhibiti kipindupindu pamoja na kuzitaka halmashauri kutunga sheria ndogo ndogo zitakazo saidia kudhibiti majitaka.

 

error: Content is protected !!